Header

Rammy Galis ashauri mchanganyiko wa Bongo Movie na Bongo Fleva

Muigizaji wa Bongo Movie aliyepamba video ya Ray C ya ‘Unanimaliza’ Rammy Galis amezungumzia faida ya mastaa wa filamu kutokea katika video za wasanii wa muziki hasa Bongo Fleva.

Akipiga stori na Dizzim Online Rammy, amesema kuwa ni faraja kwake kuonekana mwenye thamani katka tasnia ya filamu kiasi cha kupewa nafasi ya kutokea katika video ya Ray C na jambo hilo lina mchango mkubwa kwa waigizaji husika kwakuwa ni nafasi ya mashabiki kuwaona mastaa wao katika aina nyingine ya Burudani.

“Kwa mimi kushriki katika Music Video ya Ray C inatengeneza Impact kwasababu katika burudani hiyo ya muziki watu wanaweza kumuona msanii ambaye wanampenda hususani msanii wa filamu. Kwa hiyo pindi wanapokuwa wanakuona kwenye video hiyo ya muziki inatengeneza hamu na hamasa ya kuendelea kukufatilia na kupenda kuiona ile video” Amesema Rammy.

Hata hivyo Rammy ameeleza kuwa kufanya hivyo bado inaongeza hali ya ushirikiano wa tasnia mbili tofauti kitu ambacho kinawasaidia wasanii wa kutoka pande zote mbili za tasnia ya sanaa na burudani kwa ujumla.

“Vile vile kufanya hivyo hapa unatengeza kolabo ya mashabiki, yaani mashabiki wa filamu unawapata na mashabiki wa muziki wako unawapata pia kwa hiyo huo ndo mchango kwa msanii wa muziki endapo atamshirikisha msanii wa filamu katika muziki wake” Ameongeza.

Comments

comments

You may also like ...