Header

Ujerumani kinara Viwango vya FIFA, Tanzania yapanda kwa nafasi 25

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015, Ujerumani imeipiku Brazil kwa kuwa kinara katika orodha ya viwango vya timu bora za Taifa Duniani Vilivyotolewa Leo Juni 6 na shirikisho la Mpira Duniani FIFA.

Timu ya Taifa ya Ujerumani ambayo ni Bingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014, Kombe la Mabara 2017, Kombe la Ulaya kwa vijana U21 2017, wameongoza orodha hiyo kwa kuwa timu bora ya Taifa mbele ya miamba ya soka Brazil pamoja na Argentina walioporomoka kutoka nafasi ya kwanza na ya Pili.

Kwa Upande wa Afrika Timu ya Misri inaongoza ambayo katika orodha ya jumla inashikilia nafasi ya 24 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 27 pamoja na Congo DR katika nafasi ya 28 huku Timu ya Tifa ya Tanzania Taifa Stars ikipanda kwa nafasi 25 kutoka ikishikilia nafasi ya 114 toka nafasi ya 139.

FIFA imetoa viwango hivi ili kutoa taswira na kuamua katika upangaji wa Mechi za mtoano pamoja na upangaji wa Droo ya Kombe la Dunia litakalofanyika Mwakani 2018 nchini Urusi, Upangaji wa michezo ya mtoano unatarajia kufanyika Desemba 1 Mjini Moscow Nchini Urusi.

Comments

comments

You may also like ...