Header

Chemical adai kuwa tayari kujitosa kwenye movie

Msanii wa hip hop, Chemical amezungumzia mipango yake juu ya suala la uigizaji baada ya kufanya movie iliyotokana na ngoma yake ya “Marry Marry.”

Akizungumza na Dizzim Online rapper huyo wa kike amesema kuendelea kuigiza kwa upande wake sio tatizo kwasababu amesomea sanaa.

“Sanaa niliyosomea inaruhusu kufanya sanaa zote ikiwemo na uigizaji pia,” amesema. “So hata nikitaka kuendelea kuigiza bado ninayo nafasi. Muziki ni kwa vile nilianzia huko na ndio maana nimeanza kuonekana upande ule ingawa naupenda zaidi ya sanaa yeyote ile. So ikitokea katika ngoma ambazo nitatoa kama zitakuwa na ujumbe wa kuvutia zaidi nitafanyia movie,” amesisitiza.

Movie ya Marry Marry ambayo imechezwa na waigizaji wakubwa akiwemo Wema Sepetu bado haijatoka.

Comments

comments

You may also like ...