Header

Stars kujaribu nafasi ya Mwisho COSAFA

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kinashuka Dimbani hii leo Julai 7 kucheza Mchezo wa kusaka Mshindi wa tatu dhidi ya Timu ya taifa ya Lesotho katika Dimba la Moruleng kwenye Mashindano ya Kombe la COSAFA  yanayoendelea nchini Afrika Kusini.

Stars ambayo imeshindwa kutinga hatua ya Fainali baada ya kufungwa Magoli manne kwa mawili dhidi ya Zambia katika hatua ya nusu Fainali ya Michuano hiyo ambayo Tanzania ni nchi Mualikwa huku wapinzani wao Lesotho walipoteza dhidi ya Zimbabwe kwa jumla ya Magoli manne kwa matatu.

Timu hizi mbili zilikutana mwezi uliopita Juni 10 katika Mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam na kushuhudia timu hizo zikitoka sare ya goli moja kwa moja.

Michuano hiyo ya COSAFA itafikia tamati Julai 9 mwaka huu kwa Mchezo wa Fainali kati ya Zambia dhidi ya Zimbwabwe.

Comments

comments

You may also like ...