Header

Diana Edward adai Umiss Tanzania umemlainishia maisha

Miss Tanzania 2016, Diana Edward amezungumzia faida  anazozipata kutokana na umaarufu wake alioupata baaada ya kutwaa taji hilo.

Akizungumza na Dizzim Online mlimbwende huyo amesema umaarufu wake umesababisha apate msaada hata kwa watu ambao hakuwategemea kama wanaweza kumsaidia katika maisha yake

“Yaani sasa hivi napata support kubwa sana tofauti na zamani ilivyokuwa. Yaani ilikuwa shida sana kama nataka kitu kupata kwa wakati. Lakini kwa sasa naamini umaarufu wangu umechangia sana, ingawa saa zingine inanishinda kufanya vitu amavyo mimi kama mimi napend, kama kucheza mbele za watu sasa hivi nashindwa kabisa yaani kwasababu inapokelewa tofauti na jamii. Lakini mwisho wa siku hamna mtu wa kumlaumu kwasababu nilipenda mwenyewe,” amesema.

Comments

comments

You may also like ...