Header

Ray Vanny: Wanaume wenye hela wanammendea Fahyma

Jahazi la Ray Vanny na mchuba wake Fahyma aka Mama Jaydan linakumbana na sio mawimbi tu, bali mashambulio ya ‘papa’ wenye uchu baharini. Mshindi huyo wa tuzo ya BET ameiambia Chill na Sky ya Dizzim Online kuwa, wanaume kibao wanataka kumtoa kwenye umiliki wa msichana huyo mrembo.

“Kwasababu ukiangalia umri wake na alivyo, watu wengi sana wanamsumbua wengine wana hela sana, watu wengi sana wanamfuata,” amesema.

“Kwahiyo kuweza tu kuvumilia na kuweza kutulia na mimi, sometimes sio eti nampa hela nyingi au nampa vitu vingi vya kufanya eti abaki, hapana. Ana uvumilivu yaani, hana tamaa. Ni mwanamke mzuri mimi nampenda, yeye mwenyewe najua ananipenda.”

Ray amesema kitendo cha Fahyma kubeba mimba na kujifungua kimedhihirisha kuwa anampenda sababu wasichana wengi hawako tayari kuzaa na pia familia yake haikubariki sana hatua hiyo.

“Alikuwa na vita kubwa,” anasema Ray. “Sio watu wote waliomsupport kwamba aje ajifungue lakini hakuweza kusikiliza na akavumilia mpaka akaniletea Jaydan mtoto mzuri, ukimuona bado kinanda vile vile kama hajazaa.”

Comments

comments

You may also like ...