Header

Ridhiwani Kikwete awaasa waigizaji wa filamu kuzingatia maadili

Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani kikwete amewaomba wasanii wa maigizo nchini wajitambuwe na kujua kuwa  wanachokifanya ndio kazi yao na ndio maisha yao.

Akizungumza na Dizzim Online mtoto huyo wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakata Kikwete, amesema kujitambua ni kitu muhimu katika maisha ya kazi inayotaka ubunifu zaidi kama maigizo.

“Waigizaji wanatakiwa kujua kuwa uigizaji ni kazi kama zilivyo kazi zingine hivyo ni muhimu sana wakijitambua. Wafahamu uigizaji unasababisha watoto wasome, unasababisha kujulikana pia unasababisha kutupa heshima sisi na kuendesha maisha yetu kiujumla. Kwahiyo wakijua hilo ndipo uchungu utaongezeka zaidi kwa kufanya kilicho bora zaidi,” amesema.

“Ingawa serikali nayo ni lazima isaidie kusupport mazingira ambayo itasababisha kilio chao kinaisha,” amesisitiza.

Comments

comments

You may also like ...