Header

Verratti aomba radhi PSG kwa niaba ya Wakala wake (+Video)

Paris Saint-Germain's Italian midfielder Marco Verratti looks on during the French L1 football match between Paris Saint-Germain (PSG) and Rennes (SR) at the Parc des Princes stadium in Paris on January 30, 2015. AFP PHOTO / FRANCK FIFE (Photo credit should read FRANCK FIFE/AFP/Getty Images)

Kiungo wa Klabu ya soka ya PSG Marco Verratti ameomba radhi Uongozi wa klabu poamoja na Mashabiki kufuatia kauli ya Wakala wake Donato Di Campli ya kuwa kiungo huyo hana furaha nchini Ufaransa huku akionyesha wazi kuwa Verrati anaweza kuelekea Barcelona.

PSG wameweka kipande cha Video katika ukurasa wao wa Mtandao wa kijamii wa Twitter inayomuonesha Verratti, 24 akiomba msamaha kwa kauli yake pamoja na kuwahakikishia Mashabiki ataendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo alijiunga nayo mwaka 2012 akitokea klabu ya Pescara.

“Nina Furaha ndani ya Klabu hii, Kesho nitaungana na wenzangu kwenye Mazoezi. Nina hamu ya kurejea tena mazoezini, Najua timu inaniamini sana na ndio maana naomba Msahama kwao. Siongei sana kwa sababu naiheshimu sana PSG kwa sababu imenifanya niwe Mchezaji ambaye nipo sasa kiukweli naomba msamaha kutoka ndani ya Moyo wangu. Alisema Marco Verratti.

“Yale hayakuwa Maneno yangu, Kiukweli wakala wangu amefanya kosa kubwa sana, nadhani hii haitojirudia tena nitafanya kazi yangu katika klabu na nitafanya vizuri”.

 

 

Verratti ameamua kukanusha kauli aliyotoa Wakala wake alipokuwa akihojiwa na kituo cha Redio cha Dello Sport cha nchini Italia kwa kudai kuwa PSG ni Klabu ambayo haiwezi mshikilia Mchezaji na kumpa mahitaji yake yote huku akisema kuwa Verratti hana Furaha klabuni hapo na huenda akaondoka kuelekea Barcelona.

Comments

comments

You may also like ...