Header

Dr. Dre na Eminem wakutana kazini tena

NEW YORK, NY - NOVEMBER 05: (L-R) Eminem, Dr. Dre and Jimmy Iovine attend WSJ. Magazine 2014 Innovator Awards at Museum of Modern Art on November 5, 2014 in New York City. (Photo by Jamie McCarthy/Getty Images)

Taarifa njema kwa mashabiki wa muziki wa rapa kutoka Marekani ‘Eminem’ imeanza kunukia kutokana na kilichosemwa na Allan Hughes ambaye ni muongozaji wa Documentary ya hadithi ya ushirikiano wa mtayarishaji wa muziki Jimmy Iovine na Dr. Dre ‘The Defiant Ones’.

Muongozaji huyo wa filamu wa Marekani, alipokuwa akihojiwa na kituo cha habari za burudani cha Marekani cha Uproxx amesema kuwa Dre na mkali huyo wa Rap God wameungana na wanautumia muda wao mwingi studio wakiandaa kazi mpya za Eminem.

“Dre bado ana-record,” Alisema. Watu kitu ambacho hawakijui ni kwamba Dre anarecord kila siku. Hali ilivyo ni kwamba yuko studio anarecord nyimbo kila siku. Yeye ni kama Picasso, muda wote anachora. Kwa sasa hivi anatayarisha 11th hour, wimbo utakaokuwa katika album mpya ya Eminem. Hivyo Dre bado yuko kazini kimuziki” Allan Hughes Aliongeza.

Dr. Dre, Jimmy Iovine na Allen Hughes

Comments

comments

You may also like ...