Header

Khaligraph Jones alala kwenye Jeneza kufikisha ujumbe

Rapa kutoka Kenya, Khaligraph Jones a.k.a Papa Jones ameachia wimbo unaokwenda kwa jina la ‘Gaza’ wenye wazo la kujiuliza kuwa tunapoondoka duniani ni wapi tunakwenda ambapo katika video Khaligraph anaonekana akiwa ndani ya jeneza.

Wimbo huo uliotayarishwa chini ya studio zake za Blu Ink Corp ambapo bado Khali anasikika katika mjadala kati ya watu wawili, Moja aliye hai na mmoja aliyekufa tayari ambapo wote walikuwa wanachama wa kikundi fulani amabacho sio kizuri.

Aliyekufa anajaribu kumshauri mtu aliye hai kuachana na mipango yake ya kulipiza kisasi kwa kupanga kuua Afisa wa polisi waliohusika na kifo na kukubali kuwa njia aliyoishi nayo ndo imepekea kifo chake  na huyu aliyehai kama hatabadilika naye atafuata njia hiyo hiyo.

Wimbo huu wa Khaligraph unasihi vijana kila mwenye niambaya ya maisha ambayo inapigwa vita na maafisa wa polisi kuachana nayo kwakuwa hakuna faida ya kuishi katika mfumo huo wa maisha na kikubwa kinachoweza kutokea ni kifo na sio kingine.

 

Comments

comments

You may also like ...