Header

Lukaku awapa neno la Mwisho Everton

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku ambaye amekamilisha Usajili wake kujiunga na Klabu ya Manchester United akitokea Everton ameaga rasmi klabu yake ya Everton kwa ujumbe alioandika kupita kurasa zake za Mitandao ya Kijamii siku ya Jana.

Lukaku, 24 ambaye amekamilisha vipimo vya Afya siku ya Jana tayari kujiunga na United kwa ada ya Paundi Milioni 75 ameweka video ya Picha zake akiwa Everton na kuandika ujumbe mfupi wa Maandishi ambao amewashukuru Mashabiki, Uongozi pamoja na Benchi zima la Ufundi na kuwahakikishia kuwa kamwe hawezi kuisahau timu hiyo iliyomfanya Dunia imjue.

“Napenda kuwashukuru watu wote ndani ya Klabu ya Everton napenda kuwashukuru Mashabiki kwa ushirikiano wao miaka yote minne tuliyokuwa wote, kiukweli mmenipa nguvu sana katika kila Mchezo na naweza kusema ilikua safi sana kucheza Mbele yenu, Tangu siku ya Kwanza nacheza mbele yenu na mbele ya Uongozi mlinipa nguvu na kufanya nijiskie nipo nyumbani. Wachezaji wenzangu asanteni sana kwa ushirikiano wenu Benchi la ufundi asanteni pia kwa kunifanya niwe Mchezaji Mzuri kufanya kazi na nyie ilikua raha sana na naahidi kuwa nitaendelea kufata ushauri wenu katika Maisha yangu yote ya Soka. Asante sana Klabu ya Everton”.

Lukaku amefunga Jumla ya Magoli 56 katika michezo 110 ndani ya Everton na kumfanya kuwa Mchezaji aliyefunga Magoli mengi katika historia ya Klabu hiyo. Amewai tumikia Vilabu mbalimbali ikiwemo Chelsea mwaka 2011 mpaka 2014 kabla ya kupelekwa kwa mkopo Everton na baadae kujiunga moja kwa moja na timu hiyo.

 

 

Comments

comments

You may also like ...