Header

Tatoo hii kufufua moyo wa mapenzi wa Jackline Wolper

Staa wa maigizo, mjasiriamali na mpenzi wa zamani wa staa wa Bongo Fleva Harmonize ‘Jackline Wolper’ ameanza tena kuonekana katika sura mpya ya dimbwi zito la mahaba na mwanamitindo kutoka Tanzania ambaye ametambulika kwa jina lake maarufu la ‘Brown’.

Kupitia picha moja yenye uzito wa kuwa kipo kinachoendelea kati ya Brown na Wolper, Dizzim Online ilifanikiwa kuinasa picha ya kijana huyo iliyomuonesha akiwa amechora tatoo eneo la juu la kifua chake yenye maana kuwa anampenda Wolper ‘I love Wolper’.

Brown kupitia akauti yake ya Instagram siku mbili zilizopita alipost picha ya Wolper huku akiweka maneno ya kunesha kuwa ni mtu muhimu kwake.

Picha za ishara ya kuelea kwa mahaba ya wawili hao

That one person you’re so lucky to have beside you, even when everything fall #bff” Aliandika.

Brown katika Ubora wake

Kwa muonekano wa Brown na muoneano wa mpenzi wa zamani wa Wolper ‘Harminze’ ni wazi kuwa Jackline Wolper ni mtu anayependa kijana mwenye muonekano wenye pambo la tatoo kutokana na kufanana kwa baadhi ya michoro ya tatoo za Brown na Harmonize.

Tatoo ya Mkono wa Harmonize yenye mfanano na ya Brown

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...