Header

Abydad ahimiza watayarishaji wa muziki Bongo kushirikiana

Producer wa hits kibao, Abydad amesema ushirikiano baina wa watayarishaji muhimu katika kuzalisha muziki mzuri. Ameiambia Dizzim Online kuwa ushirikiano huongeza ujuzi zaidi.

“Unajua mnapokutana maproducer tofauti tofauti inakuwa ni poa zaidi kwasababu kila producer ana feeling zake, kila producer ana uwezo wake. Kwahiyo endapo mtashirikiana kwa pamoja lazima vitu vizuri vitokee. Na kwa kawaida kila producer ana uwezo wake, mimi nina uwezo wangu na wengine wana uwezo wao. Kuna kitu mimi nakifanya wenzangu hawakifahamu, so pindi mnapokutana kila mtu anaweza kupata ujuzi kutoka kwa mwenzie,” amesisitiza.

Aidha Aby aliyetayarishaji Chekecha Cheketua ya Alikiba miongoni mwa hits zingine, ameongeza, “Mnapo kuwa maproducer zaidi ya mmoja faida nyingine ni kila mtu anakuwa anaumiza akili kupata kitu kizuri zaidi na lazima nyimbo itakuwa kubwa na nzuri zaidi. Kama tunavyojua kitu chochote kinachotumia akili kwa muda mrefu lazima kiwe kizuri.”

Comments

comments

You may also like ...