Header

Hii ndio sababu ya Nandy kumfanya Ben Pol ‘boyfriend’ kwenye Wasikudanganye

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nandy ametoa sababu ya kumweka Ben Pol kama mpenzi wake kwenye video ya ngoma yake mpya ‘Wasikudanganye.’

Nandy ameiambia Dizzim Online kuwa alimuona Ben Pol kama mtu anayefit kubeba uhusika huo.

“Nimemuweka Ben Pol kwenye video kwasababu ni mtu ambaye anafiti sehemu ambayo tulimpa. Halafu mimi katika kutafuta ma video king nilikuwa nataka niwe tofauti kidogo, yaani video king awe msanii mwenzangu. So katika kuangalia nikaona Ben Pol ndiye atafaa na ataendana na mimi, na nashukuru ameitendea haki video yangu,” amesema Nandy.

Kwa upande wake Ben aliambia Dizzim kuwa alikubali kucheza uhusika huo kwenye video ya Nandy kwasababu anampenda.

Comments

comments

You may also like ...