Header

Baada ya kufunga ndoa: Bella Kombo ageukia muziki wa injili

Aliyekuwa mshiriki wa BSS mwaka 2011, Bella Kombo ambae kwa sasa ameingia rasmi kwenye muziki wa injili, amezitaja sababu zilizomfanya kuwa kimya tangu kipaji chake kilipogundulika mwaka huo.

Akiongea na Dizzim Online msanii huyo ambaye ametoa ngoma yake hivi karibuni amesema kikubwa ni mambo yake ya maisha pamoja na kufunga ndoa.

“Nilikuwa najaribu kuweka mambo yangu sawa kumaliza mambo yangu ya ndoa, kutulia na kukua zaidi kiroho kwasababu nilikuwa nafanya muziki wa kidunia na nilikuwa sijasimama vile ambavyo nataka na kuifuta ile picha ambayo watu wengi walikuwa nayo kuhusu mimi tangu kipindo kile cha BSS,” amesema muimbaji huyo. “So nikaamua kujitenga kidogo  na kukaa na Mungu kumuomba, na sasa ni wakati sahihi wa mimi kusimama tena,” amesisitiza.

Bella ametoa wimbo wake wa injili uitwao Alpha& Omega na amewahakikishia mashabiki wake kutorudi tena kwenye muziki wa kidunia.

Comments

comments

You may also like ...