Header

Baada ya Rayon Sports, Azam kumenyana na Mbeya City, Lipuli na Njombe Mji(+Audio)

Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati klabu ya Soka ya Azam Fc imekubali mualiko wa Mchezo wa kirafiki dhidi ya Klabu ya Mbeya City utakaopigwa siku ya Mbeya City Day Julai 22.

Jafari Iddi Maganga ambaye wa Msemaji wa Azam Fc amethibitisha kupokea na kukubali mualiko wa Mbeya City mara baada ya timu yao kurejea kutoka Rwanda.

“Tumepata Mualiko kutoka Klabu ya Mbeya City ambao wana Mbeya City day kwaiyo wameona ni vyema kuialika Azam Footbal Klabu ili iweze kuchea nao katika Sherehe zao na Azam imekubali kuwasapoti Mbeya City na Mchezo huo tunatarajia kuucheza mnamo tarehe 22 Mwezi huu katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya”. Jafari Iddi Maganga.

Aidha Azam itacheza Mechi ya Kirafiki na Timu ya Njombe Mji ya Mkoani Njombe pamoja na Lipuli Fc ya Mkoani Iringa ambazo zimeomba Mualiko pia wa Azam FC.

 

 

Comments

comments

You may also like ...