Header

Wanasheria wa Blac Chyna wampania ex wake mwingine mwenye picha na video za utupu

Mandatory Credit: Photo by REX/Shutterstock (8928731c) Blac Chyna Blac Chyna restraining order court hearing, Los Angeles, USA - 10 Jul 2017

Blac Chyna ameingia vitani dhidi ya maex wake akiwemo mzazi mwenzake, Rob Kardashian. Timu yake ya wanasheria imempania ex wake mwingine aitwaye Ferrari ambaye anadaiwa kuwa na picha za utupu za Chyna, 29, ambazo anataka kuzisambaza kinyemela.

“Tunafanyia kazi kuchukua hatua dhidi ya Ferrari,” wakili wa Chyna, Walter Mosely aliiambia PEOPLE. “Amekuwa akichapisha video za Chyna akiwa amelala. Tunaichukulia kwa umakini sana.”

“Ni mtu ambaye alikuwa na uhusiano naye wa muda mfupi miezi iliyopita na anataka kuuongeza umaarufu wake wa dakika 15. Ni rapper mchanga na atafuta mwanga katika suala zito. Tumemuomba aache kuwasiliana naye [Chyna].

“Kwa sasa [Chyna] amejikita kulea watoto wake na kuboresha biashara yake. Hatafuti mapenzi ama kuwa na uhusiano na mtu.”

Wiki iliyopita, Chyna na mwanasheria wake Lisa Bloom walitangaza kusaka zuio dhidi ya ex wake, Rob Kardashian kumsogelea baada ya kupost picha na video zake za utupu akimtuhumu kwa uashareti.

Comments

comments

You may also like ...