Header

Alves amkimbia Guadiola ajiunga na PSG

Beki wa kulia kutoka Brazil Dan Alves amekamilisha Usajili wa Miaka Miwili katika Klabu ya PSG akitokea Juventus Turin Bure baada ya kusitisha Mkataba wake na Juventus baada ya kumalizika kwa Msimu Uliopita.

Awali Alves, 34 aliripotiwa kutaka kujiunga na Kocha wake wa Zamani wa Pep Guadiola ambaye anaifundisha Klabu ya Soka ya Manchester City, Ingawa taarifa kutoka Nchini Ufaransa zinaeleza kuwa PSG wamepanda dau mara mbili ya lile waliloahidi Man City kumlipa Mchezaji huyo kwa Wiki.

Manchester City ambao inaripotiwa waliahidi kumlipa Mchezaji huyo Paundi 115,000 kwa wiki Matajiri wa jiji la Ufaransa PSG wamepanda dau mpaka paundi Milioni 240,000 kwa wiki kwa Mchezaji huyo wa Zamani wa Sevilla pamoja na Barcelona.

Dani Alves ameshinda Jumla ya Mataji 33 akiwa na Vilabu tofauti ikiwemo ubingwa mara tatu wa UEFA champions Ligi mara tatu akiwa Barcelona. Beki huyo anaungana na Wabrazil wengine katika klabu hiyo akiwemo Thiago Silva, Marquinos pamoja na Lucas Moura,

 

 

Comments

comments

You may also like ...