Header

Malaika: Sina mpango na ndoa

Malaika hana mpango na kitu kinachoitwa ndoa, walau kwa sasa.

Akizungumza na Dizzim Online Malaika amesema kutokana na mateso aliyoyapata kwenye mahusiano yake yaliyopita hafikirii kuja kuolewa hivi karibuni.

“Kwa watu wanaofuatilia kazi zangu, nadhani watakuwa wanafahamu kwamba mwaka mmoja uliopita niliweza kuachana na mtu ambaye alikuwa mpenzi wangu. Nilijifunza vitu vibaya sana na hii haimaanishi  kwamba alikuwa anafanya vitu vibaya peke yake, alikuwa na mema yake kama binadamu, lakini mimi kama mimi kutokana na hayo kwa sasa inakuwa ngumu sana kufikiria ndoa,” amesema.

Aidha aliongeza na kusema, “Ndoa ni kitu kikubwa sana, tukae tukijuwa ndoa sio mnaoana leo halafu kesho mnaachana hasa katika ndoa zetu za kikristo. Naheshimu sana ndoa na sitaki kukurupuka kwasababu ya kuwafurahisha walimwengu.”

Comments

comments

You may also like ...