Header

Barack Obama na Donald Trump kushuhudia pambano la Mayweather na McGregor

 Bondia maarufu Floyd Mayweather amesema upo uwezekano wa Rais msataafu na Rais wa sasa wa Marekani aliyeko madarakani kuhudhuria pambano baina yake na  McGregor.

Katika kulisubiri pambano lao litakalofanyika tarehe 26 Augusti, Rais Barack Obama na Donald Trump wanauwezekano wa kuhudhuria pambano hilo kwa mujibu wa Matweather. Ni majuzi tu Mayweather alishatambiwa kutandikwa na McGregor ambapo sasa hivi Mayweather amejihakikishia kushinda mchezo huo kwakuwa anaamini ni aina ya michezo ambayo amekuwa na historia ya kushinda.

“Obama anaweza kuwepo, Donald Trump anaweza kuwepo pia. nika uhakika litakuwa ni pambano na tukio la kubwa” Mayweather aiambia TMZ.

Hata hivyo Mayweather katika kutamba kuhusu ukubwa wa pambano hilo ameongeza kuwa mpaka sasa amaebadilisha namba yake ya simu ya mkononi kutokana na idadi kubwa ya watu ambali mbali kumtafuta kwa hitaji la tiketi ya pambano hilo.

Comments

comments

You may also like ...