Header

Lacazete, Rooney waanza Vyema Pre-Season

Timu ya Arsenal pamoja na Everton zimeanza vyema mechi zao za maandalizi kwaajili ya Msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi katika Michezo yao ya kwanza huku Washambuliaji wao waliosajiliwa dirisha kubwa la Usajili wakianza vyema ndani ya Timu zao.
Mfaransa Alexandre Lacazzete ambaye amesajiliwa na Arsenal Wiki moja iliyopita ameanza vyema katika klabu ya Arsenal baada ya kufunga goli lake la kwanza katika Ushindi wa mabao mawili kwa sifuri kwenye Mchezo dhidi ya Sydney Fc likiwa ni Goli lake la kwanza tangu ajiunge na Arsenal akitokea klabu ya Lyon.
Wayne Rooney ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani ya Everton akitokea Manchester United alifunga goli la kwanza katika ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika Mchezo wa kirafiki uliopigwa Jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.
Arsenal ipo nchini Australia ambako imeweka kambi kwaajili ya kujiandaa na Msimu ujao 2017/2018 kabla ya kurejea nchini England ambapo itaanza kutupa karata yake katika Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Leicester City Agosti 11 huku klabu ya Soka ya Everton ambayo ipo Tanzania itaanza Mchezo wake wa kwanza dhidi ya Stoke City Agosti 12.

Comments

comments

You may also like ...