Header

Exclusive: Nasty C asimulia mama yake alivyouawa kipindi ana miezi 11 tu tangu azaliwe

Rapper wa Afrika Kusini, Nasty C alimpoteza mama yake akiwa na umri wa miezi 11 tu tangu azaliwe, ameiambia Dizzim Online. Mama yake huyo alifariki kwa kupigwa risasi. Kwenye mahojiano nasi wiki hii jijini Dar es Salaam, rapper huyo anayetokea Durban amesema:

Kilichotokea ni kwamba mama yangu alikuwa anatoka kazini, alikuwa anafanya kazi Johannesburg, nilikuwa nakaa na baba yangu na ndugu zangu Durban. Kuna kitu kilitokea kwa dada yangu, mwanae hivyo ikambidi arudi haraka nyumbani wikiendi hiyo, lakini kwasababu alikuwa na wasiwasi sana, alitaka kuwahi kufika kama Jumatano, wakati anawahi ni kama alikuwa katika sehemu isiyo sahihi, muda usio sahihi katika taxi isiyo sahihi na kulikuwa na kama ugomvi wa taxi basi ikawa bahati mbaya

Nasty ametoa nyimbo kadhaa kuomboleza kifo cha mama yake ukiwemo wa hivi karibuni UOK, uliopo kwenye album yake ya kwanza, Bad Hair.

Comments

comments

You may also like ...