Header

Riky Rick zamu yake ya kuendelea kufanya vizuri

Rikhado Makhado a.k.a Riky Rick ni mkali kutoka Afrika ya Kusini aliyepata zaidi heshima kupitia muziki wa rap mwaka 2015 baada ya kuachia album yake ya kwanza ya ‘Family Values’.

Ricky anafahamika kwa mtindo wake wa kuficha jicho lake moja ingawa kwa sasa amepumzisha kujitokeza akiwa katika muonekano huo. ;Mwishoni0 mwa mwaka 2013 aliachia ngoma yake ya ‘Amantombazane’ ikafanya vizuri kisha remix yake iliyofanya vizuri zaidi kwa ushiriki wa marapa wakali wa Afrika Kusini kama vile Okmalumkoolkat, Maggz, Gingerbread Man, Nadia Nakai, Dj Dimplez, Kwesta na Da Kid-X na leo Ricky ni tarehe yake muhimu sana kwakuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na anatimiza umri wa miaka 30.

Kingine cha pekee kuhusu rapa Ricky hasa katika muziki wake ni ujio wake wa mwezi Mei mwaka huu ambapo ameachia mixtape yake ya tatu inayokwenda kwa jina ‘Scooby Snacks’ yenye idadi ya ngoma 3 ambayo imemshirikisha msanii mmoja pekee wakuitwa Frank Casino kupitia wimbo wa ‘Familly’.

Comments

comments

You may also like ...