Header

Harmonize aiwasha kwa mara nyingine Nyota ya Mr. Nice

Msanii wa muziki na mkali wa miondoko ya TAKEU Lucas Mkenda a.k.a Mr. Nice, nyota yake imewashwa kwa mara nyingine kupitia kwa msanii wa lebo ya muziki ya WCB ‘Harmonize’ kwa kumtumia katika somo la kupanda na kushukwa kwa maisha ya kila siku.

Harmonize katika ujio wa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Sina’ amemtumia Mr. Nice katika video ya wimbo huo kama muigizaji mkuu wa simulizi ya kisa kinachoelezea kushuka kwa kimaisha na kupoteza marafiki pindi mtu anapoishiwa.

Hata hivyo baadhi ya walioona ushirikiano huo wamepata nafuu ya kungoja kazi nzuri kutoka kw Mr. Nice baada ya kuona ujio huu na kuhusika kwake kwakuwa mmiliki wa lebo ya Muziki wa WCB ‘Diamond Platnumz’ alishaweka wazi uwezekano wa kumsaidia na kumrudisha Mr. Nice kama atakuwa tayari.

Comments

comments

You may also like ...