Header

Darassa: Wanaosema Hasara Roho haijahit, wanitaje ipi imehit kuizidi!

Msanii wa muziki wa kizazi Hip Hop nchini,  Darassa ameamua kuwatolea uvivu wale wanaosema ngoma yake , Hasara Roho haijafanya vizuri ukilinganisha na zingine zilizopita.

Akipiga story na Dizzim Online staa huyo wa ngoma ya Muziki amesema mpaka sasa hivi haelewi watanzania wana matatizo gani kwenye muziki.

“Ngoma yangu haijafanya vizuri ya nani imefanya vizuri? Nataka wanitajie wimbo ambao umevunja rekodi ya Darassa toka umetoka, lakini ukija kushindanisha Darassa wa Muziki na  Darassa wa Hasara Roho unafanya utani kwenye kioo. Ninachojua mimi ngoma yangu imefanya vizuri na mpaka sasa inafanya vizuri,” amesisitiza.

Muziki ndio wimbo wa Darassa uliofanya vizuri zaidi kuliko zote alizowahi kufanya.

Comments

comments

You may also like ...