Header

‘Johnny’ ya Yemi Alade yagonga mamilioni ya watazamaji

Msanii, mrembo na staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Yemi Eberechi Alade a.k.a Yemi Alade amevunja record ya video ya muziki Afrika kwa video ya wimbo wake wa ‘Jonny’ kufikisha watazamaji zaidi ya millioni 70. tangu ilipotoka rasmi.

Video hiyo iliyopandishwa katika mtandao wa Youtube March 3, 2014 inatajwa kuwa kati ya kazi za Yemi Alade zinazopendwa zaidi kiasi cha kufikia mafanikio ya kutazamwa na watu wengi zaidi ikilinganishwa na video za kazi nyingine za wasanii ambazo zimeonekana kufanaya vizuri kwa kipindi cha kutoka kwake mpaka sasa .

Hata hivyo katika biashara za mtandaoni hasa kwa wasanii kupitia kuweka kazi zao za picha, kazi ya  ‘Johnny’ iliyotayarishwa na Selebobo inaweza kuwa moja ya kazi iliyowaigizia pesa ndefu kutokana na mapokea yake na inaweza kutajwa kama video ya msanii wa kike kutoka Afrika kuwahi kutazamwa zaidi.

Comments

comments

You may also like ...