Header

Nick wa Pili awashauri waongozaji wa video Bongo kutoigana

Mwana hip hop kutoka Weusi Company, Nick wa Pili amesema ili waongozaji wa video za muziki hapa nchini waweze kufanikiwa, ni lazima waepuke kuigana.

 

Ameiambia Dizzim Online, “madirector wa Bongo wanachangamoto ya video kufanana, idea kufanana  au aina ya vitu ambavyo vinakuwa kwenye video kufanana.”

“Mimi nafikiri uwanja wa video ni mpana sana,  nafikiri suala la imagination kiwe kitu kikubwa kwao  yaani ukiamua kuimagine hautashindwa kitu chochote. So nawaomba madirector  wajaribu kuimagine, wajaribu kufanya kitu ambacho  mtu mwingine hajakifanya  au yeye hajawahi kukifanya zamani,  yaani mpaka rangi za video zinafanana hii kitu sio nzuri kabisa na inawashusha viwango.”

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...