Header

Unahitaji dola 150,000 za kimarekani kuwaona Mayweather na McGregor

Tiketi kwaajili ya Pambano la ngumi kati ya Mabondia Floyd Myweather dhidi ya Conor McGregor zimetangazwa kuanza kuuzwa huku bei ya tiketi ikiwa ni Dola za kimarekani 150,000.

Thamani ya pambano hili inatajwa kuwa ni kubwa zaidi kuwai kutokea katika Historia ya Mchezo huu wa ngumi utakaofanyika Agosti 26 Mwaka huu 2017 katika Ukumbi wa T-Mobile Arena ambao utaingiza idadi ya watu elfu ishirini uliopo mjini Las Vegas nchini Marekani.

Mayweather, 40 atarejea tena uwanjani baada ya kutangaza kustaafu Mchezo huo wa ngumi kupambana na Conor McGregor, 29 ambaye litakua ni pambano lake la kwanza kubwa na la kimataifa. Mabondia hao wanatarajia kupata kiasi cha Dola za kimarekani 100.

Comments

comments

You may also like ...