Header

Victoria Kimani aachia kolabo yake na kundi la Marekani kama zawadi ya Birthday

Msanii wa muziki wa kiazai kipya na mzaliwa wa Marekani mwenye asili ya nchi ya Kenya Victoria Kimani, baada ya ngoma yake ya Lover aliyomshirikisha rapa Phyno kutoka Nigeria na nyingine kadhaa sasa amedondosha zawadi ya ngoma katika siku ya kumbukumbu ya kuazaliwa wake.

Katika kutimia umri wa miaka 32, Victoria Kimani ameachia kazi yake mpya aliyoshirikiana na kundi la nchini Marekani linaloundwa na ndugu wawili, Theron na Timothy Thomas ‘Rock City’ inayokwenda kwa jina ‘China Love’.

Ngoma hiyo kama njia yake ya kusherehekea siku hii muhimu kwake na zawadi kwa mashabiki imetayarishwa na Drey Beatz ambaye mbali na ujuzi wa utayarishaji wa muziki pia ni msanii anafanya vizuri kupitia kazi yake ya ‘Jungle Don Mature’ iliyotoka mwaka huu.

Isikilize hapa chini.

      Victoria-Kimani-China-Love-Ft.-Rock-City

Comments

comments

You may also like ...