Header

Unbothered: Diamond awajibu wanaoponda ‘mapumziko’ yake na Zari, Mombasa

Diamond na mchumba wake Zari wamesababisha povu la kiwango zaidi ya Omo kwa video zao wakiajichia kwenye mapumziko yao mjini Mombasa, Kenya.

Siku yote ya jana, mastaa walikuwa wakishare video kupitia Snapchat na Instagram Live kuonesha wanavyofurahia mahaba yao baada ya msiba wa mama yake Zari. Baadhi ya watu wamewakosoa kuwa ni mapema mno kujiachia hivyo, siku chache tu baada ya kumzika mama yao.

Diamond amewajibu:

Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu…. Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia… Pambaneni na Mahusiano yenu…! Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya kwanza 😛

Comments

comments

You may also like ...