Header

Arnold Schwarzenegger achukua zawadi ya mwaka mwingine

Staa wa filamu, mtunisha misuli na mwanasiasa maarufu kutoka nchini Marekani Arnold Schwarzenegger leo ni siku ya kumbu kumbu kwake na amelamba karata nyingine ya kutimiza umri wa miaka 70.

Staa huyo aliyepata umaarufu mkubwa kupitia filamu ya ‘The Terminator’ alionekana kujiingiza zaidi katika nyanja za siasa ambapo ameishaingia katika vitabu vya historia ya nchini ya Marekani kwa kuongoza kama Gavana wa jimbo la Califonia.

Kupitia mazoezi ya kunyanyua vyuma venye uzito na utunishaji Misuli Schwarzenegger yuko katika orodha ya washindi wa wa Mr. Universum kwa takriban mara saba na katika siku yake hii muhimu miongoni mwa mmarafiki na mastaa wenzake walioonekana kumtakia maisha marefu na yenye Baraka tele ni muigizaji Sylvester Stallone kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Comments

comments

You may also like ...