Header

Wizkid atumia masaa 48 kuandaa Album

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria mwenye makazi yake Marekani, Wizkid baada ya ngoma kadhaa alizoachia akiwa katika ushirikiano na mastaa wakubwa wa Marekani na Dunia, imeonekana kuwa ameingia nchini Nigeria kimuziki zaidi na kuhusika katika kuandaa album ndani ya masaa 48.

Kupitia ukurasa wa twitter wa mshikaji wake na Wizkid  @RotimyRudeBoi alipost ujumbe wa kuelezea kilichofanyika studio huku akibainisha kuwa Wizkid yuko nchini Nigeria na yametumika masaa 48 kwa kuandaa album ambayo siku sio nyingi itatoka rasmi.

Baada ya taarifa hiyo, Wizkid pia alithibitisha kutumia msaa hayo studio kuandaa kazi na muda uliofuata @RotimyRudeBoi alishindilia kwa kusema kuwa ndani ya msaa machache Wizkid anaachia wimbo mpya.

Muda uliofuata Wizkid aliachia ngoma iliyokwenda kwa jina la Medicine chini ya utayarishaji wa Masterkraft na imebainika kuwa ndani ya masaa 24 ameweza kurecord nyimbo zisizo pungua sita na kuachia moja.

Hata hivyo Wizkid ni msanii ambaye mpaka sasa anatazamwa sana na mashabiki wa muziki ndani na nje ya Afrika kwa kasi yake ya jinsi anavyoshirikiana na mastaa wakubwa katika muziki wake kama vile Drake, Trey Songz, Chris Brown na wengine kibao.

      WIZKID-MEDICINE

 

 

Comments

comments

You may also like ...