Header

Cassper Nyovest aachia video ya kolabo yake na Staa wa Marekani

Rapa kutoka Afrika ya Kusini Refiloe Maele Phoolo a.k.a Cassper Nyovest baada ya kudondosha album yake ya tatu inayokwenda kwa jina ‘Thuto’, kutoka katika album hiyo ameachia video ya wimbo unaokwenda kwa jina ‘Destiny’ wimbo uliomshirikisha staa wa kike wa muziki wa RnB na Soul kutoka Marekani ‘Goapele’.

 

Wimbo huo ulioandaliwa kwa unshirikiano wa rapa mwenzake kutoka Afrika kusini ANATII, Alie Keys na Cassper Nyovest mwenyewe ni wimbo wa pili kutoka katika album hiyo ya ‘Thuto’ kwa Cassper kumshirikisha staa huyo wa Marekani ‘Goapele’ kwakuwa ameshirikishwa pia katika wimbo wa ‘Confused’.

Cassper na Goapele

Hata hivyo mbali na album yake kuonekana kuwa inafanya vizuri katika mauzo na mapokezi, Cassper anasubiriwa kwa hamu katika ujio wa kolabo yake na rapa wa Marekani French Montana kwasababu wameishazama studio na wakaandaa ngoma ambayo inategemewa kupewa jina la ‘Wavy Fun’ na ngoma hiyo kwa mujibu wa Cassper alibainisha kuwa iko katika maadhi ya kuwafanya wapenzi wa muziki wacheze zaidi.

Comments

comments

You may also like ...