Header

Habari njema kwa wanaosubiria muendelezo wa filamu ya Avatar

Studio ya Visual effects, Weta Digital imeanza kufanyia kazi filamu nne mpya za Avatar zinazoongozwa na James Cameron. Avatar ni miongoni mwa filamu iliyoingiza fedha nyingi zaidi katika muda wote.

Kampuni hiyo yenye makazi yake nchini New Zealand ndiyo iliyohusika pia kutengeneza filamu ya War for the Planet of the Apes na imejipatia sifa kubwa katika kazi hiyo.

Filamu ya kwanza ya Avatar ilitoka December 10, 2009. Ilitumia bajeti ya dola milioni 237 na kuingiza kiasi cha dola bilioni 2.788.

Filamu nyingine nne za Avatar zitatoka kuanzia mwaka 2020, 2021, 2024 na 2025.

Comments

comments

You may also like ...