Header

Lil Uzi ngoma yake yapanda mauzo ya Platnum mara Tatu

Rapa wa kimarekani Symere Woods a.k.a Lil Uzi ambaye alianza kupata sikio la mashabiki wa muziki na wadau kupitia mixtape yake ya ‘Luv Is Rage’ iliyoachiwa Octoba mwaka 2015, ameandika historia katika muziki wake kupitia ngoma yake ya ‘XO Tour Llif3’ kwa kuthibitishwa kufikia Platinum mara tatu ndani ya miezi minne.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram rapa Uzi aleweka ujumbe wa furaha ya mafanikio ya ngoma yake hiyo kwa kuandika “I died and came back wit 3 lives⚰️®..2” kwenye picha inayoonesha kuwa wimbo wake huo umepewa heshima ya mauzo ya Platnum mara tatu.

Wimbo huo “XO Tour Llif3” umeingia sokoni rasmi mwezi Machi na mapema Aprili ulianza kufanya vizuri kwenye chati ya Billboard Hot 100 na kwa mara ya kwanza ulifikia mauzi ya nakala milioni moja yaani ‘Platinum’ mwezi Juni.

Hata hivyo ngoma hiyo iliyotayarishwa na na Producer TM88 iko katika mfumo wa video mbili sasa ambazo zimeachiwa ikiwa ni pamoja na toleo la Uhuishaji(Animation) na video ya lyrics. Upande mwingine wa maisha ya Uzi ni kwamba leo ni siku ya furaha kwake kwakuwa anasherehekea kumbukumbu ya tarehe ya kuzaliwa kwake kwa kutimiza umri wa miaka 23.

I died and came back wit 3 lives⚰️🦇®..2

A post shared by 16 (@liluzivert) on

Comments

comments

You may also like ...