Header

Manchester United yapigwa faini, Daley Blind na Jones watiwa Hatiani

Beki wa Manchester United Phil Jones amefungiwa mechi mbili na UEFA huku Daley Blind akipigwa faini baada ya kukiuka maadili ya sheria ya kufanyiwa vipimo vya dawa za kuongeza nguvu baada ya Mchezo wa Fainali ya Europa Mwezi Mei.

Jones, 25 amekutwa na hatia ya kutoa lugha mbaya na kutoonyesha ushirikiano dhidi ya maofisa baada ya kuambiwa akafanyiwe vipimo huku Beki mwezie Daley Blind amepigwa faini ya Paundi 4,450 baada ya kukutwa na hatia ya kusita kufanyiwa vipimo kwa kile kilichodaiwa kutaka kubaki na kikosi cha United kushangilia Ubingwa wa Europa.

Phil Jones ataukosa Mchezo wa Super Cup dhidi ya Real Madrid utakaopigwa Agosti 8 pamoja na ule wa makundi ya UEFA mwezi Septemba, anaungana na Beki Eric Bailly amabaye atakosa Michezo miwili pia baada ya kupata kadi nyekundu kwenye Mchezo wa nusu Fainali ya Europa.

Manchester United imepigwa faini ya Paundi 8950 baada ya kushindwa kuhakikisha Wachezaji wake wanafanyiwa vipimo hivyo. UEFA imetoa siku tatu kwa Manchester United kukata rufaa.

 

Comments

comments

You may also like ...