Header

Vanity Fair wamuingiza chaka Angelina Jolie

Angelina Jolie amekanusha vikali taarifa yake kwenye jarida la Vanity Fair iliyotafsiriwa vibaya kuhusu kuwafanyia uhuni watoto wa Cambodia walioshiriki kwenye filamu yake. Muigizaji huyo alichukua watoto wa nchi hiyo kuigiza filamu iitwayo First They Killed My Father.

Alizungumza na Vanity Fair kuhusu filamu hiyo na jinsi walivyofanya ujanja wa kuwapa hela watoto ili waigize na kisha kuzichukua. Mahojiano hayo yamesababisha hasira kubwa na Jolie anaonekana ni mnyonyaji. Kwenye mahojiano hayo, Jolie anaeleza jinsi waongozaji walivyozungumza kwenye makazi duni kutafuta waigizaji hasa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Jolie, aliyeongoza filamu hiyo ya Netflix amesema imemkera jinsi walivyo walivyotafsiri vibaya mchakato wake wa kupata waigizaji.

“I am upset that a pretend exercise in an improvisation, from an actual scene in the film, has been written about as if it was a real scenario,” amesema Jolie.

“The point of this film is to bring attention to the horrors children face in war and to help fight to protect them. The suggestion that real money was taken from a child during an audition is false and upsetting. I would be outraged myself if this had happened. Every measure was taken to ensure the safety, comfort and well-being of the children on the film starting from the auditions through production to the present,” aliongeza.

Hizi ni picha zingine za Jolie kwenye Vanity Fair:

Comments

comments

You may also like ...