Header

Beka Flavour akanusha uwepo wa bifu kati yake na Aslay

Staa wa ngoma ya ‘Libebe’ na mmoja kati ya wakali waliokamilisha idadi ya wasanii wanne wa kundi la Yamoto Band ‘Beka Flavour’ ametolea maelezo ya kile kinachozungumziwa zaidi kuhusu kutokuwepo kwa maelewani kati yake na msanii mwenzake Aslay.

Akipiga Stori na Dizzim Online Beka amesema kuwa wapo baadhi ambao wanatafsiri uwepo wa ugomvi kati yake na Aslay kitu ambacho amekanusha uwepo wa hali hiyo na kusisitiza kuwa hakuna tatizo lolote kati yao na anaamini mashabiki wanaoelewa uwezo wao na kufatilia muziki wanapata pata wanachokitaka kutoka kwao na sio vinginevyo.

“Mimi na Aslay hatuna tatizo kabisa yaani, naona mambo mengi yanazungumzwa hasa mitandaoni lakini wanaosema kuwa tunatatizo wanakosea sana. Kingine mimi na Aslay ni zaidi ya ndugu pia ukizingatia ni msanii mwenzangu ambaye naheshimiana naye na mimi sijawahi kuwa na tatizo naye hata kidogo” Amesema Beka.

Umoja wa kundi la Yamoto Band

Hata hivyo katika mhojiano tofauti Aslay naye amekuwa akitoa maelezo yanayoendelea kuonesha kuwa kila mmoja anamkubali mwenzake na hakuna tatizo balo kinachoendelea ni maneno na vitu vinavyotengenezwa na wanaotafuta cha kuzungumza kuhusu wao na muziki wao.

Comments

comments

You may also like ...