Header

Dj Walshy Fire wa kundi la Major Lazer ashirikiana na Dj D-Ommy

Dj wa kimataifa kutoka Tanzania ‘Dj D-Ommy’ ameachia mixtape ya mchanganyiko wa nyimbo(Mixing) aliyomshirikisha Dj wa kimataifa kutoka Jamaica anayeunda kundi la Major Lazer ‘Dj Walshy Fire’

F

Dj Walshy Fire

Akizungumza na Dizzim Online Dj D-Ommy ameweka wazi hatua yake ya kukwea kimataifa zaidi kwa haina hii ya ushirikiano  katika kazi ya aina yake na kumshukuru zaidi Staa wa kike wa muziki wa Bongo Fleva ‘Vanessa Mdee’ kwa kufanikisha na kuwa chanzo cha mawasilianao mpaka kufikia hatua ya kufanya kazi yao hiyo ya ushirikiano.

Mixing hiyo ya Dj D-Ommy ambayo katika kushirikiana kwa wawili hao wamehusika katika uchanganyaji wa nyimbo huku pia Dj Walshy Fire akisikika kwa sauti ya kunogesha na kutia vionjo katika mchanganyiko wa nyimbo. Mixtape hiyo iliyopewa jina la ‘Afro Caribbean’ imeachiwa rasmi Jumatatu ya tarehe 31 mwezi wa Julai.

Hata hivyo Dj D-Ommy mwkaa huu moja ya mafanikio kwake ni kukutana na wakali wengine katika kipingele cha ‘Best Dj Africa’ katika orodha ya Ma-Dj wanaowania tuzo ya Afrimma 2017 ambapo amewekwa katika kipengele hicho na madj kama vile DJ Spinall(Nigeria), DJ Joe MFalme(Kenya), DJ Black Coffee(South Africa), DJ Exclusive(Nigeria), DJ Kalonje(Kenya), DJ Paulo Paulo Alves(Angola), DJ Crème Delacreme(Kenya) na DJ Nyce(Ghana).

 

Comments

comments

You may also like ...