Header

Joh Makini aeleza kwanini ni muhimu msanii kubadilika katika nyimbo

Joh Makini amesema ili msanii aweze kudumu, ni muhimu awe na uwezo wa kubadilika katika kila nyimbo Rapper mpole kutoka Arusha, amesema hicho ndicho amekuwa akijitahidi kufanya siku zote.

“Mimi naamini msanii anaweza kubadilika  vyovyote vile anavyotaka yeye ilimradi tu afanye vizuri katika kile anachokifanya,” ameiambia Dizzim Online. “Hakuna mipaka ya kumzuia msanii kwasababu huu ni ulimwengu wa creativity so vyovyote msanii anaweza kubadilika kama atafanya vizuri basi inaruhusiwa,” ameongeza.

Joh kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake Kata Leta aliomshirikisha Davido.

Comments

comments

You may also like ...