Header

Justin Bieber kupumzisha muziki kwa lengo la kumrudia Mungu

Staa wa muziki kutoka Canada, Justin Drew Bieber ‘Justin Bieber’ baada ya taarifa za wiki iliyopita kuwa kuna mabadiliko katika ziara yake ametoa sababu ya kukatishwa kwa maonesho ya matamasha ya ziara hiyo ya ‘Purpose World Tour’ iliyoanza rasmi Machi 2016.

Akitoa sababu za kwanini amechukua maamuzi ya kukatisha show zake zisizopungua 14 ambazo zilitarajiwa kufanyika kwa tarehe tofauti tofauti huko Asia na Amerika ya Kaskazini, Bieber amewaambia waandishi kuwa yukoo sawa na kikubwa ambacho kimepelekea kukatisha show hizo ni hitaji lake la kumpumzika na utulivu kwa sasa na ziadi kuwa awe karibu na Mungu kiimani zaidi.

“Yeah I’m fine. Just resting and getting some relaxation. We’re gonna ride some bikes.” Amesema  Justin Bieber kwa maripota wa Santa Monica mjini California.Hata hivyo mpaka sasa Justin Bieber ameshafanya maonyesho yasiyopungua 150 ndani ya Mabara Sita na kwa mujibu wa Meneja wa Justin ‘Scooter Braun’ ameomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza na kuongeza kuwa wamemeheshimu hitaji la msanii wao kukatishwa kwa show ji katika kumsikiliza msanii na uhitaji wake wa kuwa karibuni na upande wa imani yake lakini ratiba itapangwa tena na mashabiki wataendelea kupata burudani tena.

Comments

comments

You may also like ...