Header

Claud asimulia alivyokutana na mke wake wa sasa

Claud amesema mke wa sasa, Mina alikuwa shabiki mkubwa wa kazi zake, kabla ya kukutana, kupendana na kufunga ndoa. Akiongea kwenye Chill na Sky, Claud ambaye jina lake halisi ni Issa Musa, amesema miaka mingi iliyopita, alikutana na Mina na akamweleza jinsi anavyopenda kazi zake lakini alivyomuomba namba ya simu, Mina alichomoa. Ameeleza kuwa baada ya hapo ilipita miaka mingi ndipo wakaja kukutana tena kupitia Facebook.

“Na mpaka leo nasema asante Facebook,” amesema Claud. “Kwahiyo tukaanza hapo chat, chat tunasalimiana, tumeenda mpaka Mungu akaja akatukutanisha tumefunga ndoa,” ameongeza na kudai kuwa walifunga ndoa Zanzibar.

Baada ya kufunga ndoa, Mina aliendelea kuishi Sweden na hivyo kumlazimu kuja Tanzania kila apatapo likizo. Hata hivyo aliamua kufanya utaratibu wa Claud kuhamia nchini Sweden ambako kwa sasa wote wanaishi huko.

Kabla ya hapo Claud alikuwa na mke mwingine lakini baadaye anasema kuna vitu ambavyo aliona haviendani naye na kuamua kuachana naye.

Comments

comments

You may also like ...