Header

Tory Lanez akamilisha album yake ya Pili

Muimbaji mwenye uwezo wa kuchana bila hata ya kaundika(Freestyle) kutoka Kanada Daystar Peterson a.k.a Tory Lanez ameweka wazi kumalizika kwa album yake na kuwasihi mashabiki kukaa mkao wa kula kwakuwa ni ujio wenye mapishi ya kazi za mchanganyiko wa maadhi tofauti tofauti ya aina ya muziki anaofanya.

Ikiwa imebainishwa na yeye mwenyewe, itakumbukwa awali mwishoni mwa mwezi Jana Tory alishatupia ujumbe katika mtandao kupitia akaunti yake ya twitter kwa kuonjesha kuwa yuko katika upishi wa album mpya ambapo aliwezakutaja moja ya msitari iliyoko katika wimbo utakaopatikana katika orodha ya nyimbo zitakazo kamilisha album.

Tory katika kuweka msisitizo zaidi kupitia ukurasa wake wa twitter kwa mara nyingine aliizungumzia album ambayo haikuwa imetolewa maelezo ya kina zaidi kwa kusema kuwa sasa imekamilika.

Hata hivyo mashabiki wa Tory ambao wameshajiweka tayari kusikiliza ni kipi kimeandaliwa katika Album hiyo ambayo imetaarifiwa kumalizika, kwa sasa wanaendelea kufurahi ushirikiano wake na Trey Songz katika marudio ya wazo huku wakibalidilisha ushairi na baadhi ya melody zao za hit song ya rapa Dj Khaled iliyowashirikisha Rihanna na Bryson Tiller ‘Wild Thoughts

 

Comments

comments

You may also like ...