Header

Wanawake wawili na mwanaume mmoja wajitokeza kudai kuambukizwa gonjwa la zinaa na Usher

Huu si mwaka mzuri kwa Usher. Skendo yake ya kuambikiza watu gonjwa la zinaa imezidi kupamba moto. Sasa watu watatu wengine wamejitokeza na kudai aliwaambukiza ugonjwa herpes. Wapo wanawake wawili na mwanaume mmoja.

Wote wanadai kuwa Usher hakuwaambia kuwa ana gonjwa la zinaa kabla ya kufanya nao mapenzi, kwa mujibu wa TMZ. Wote wanawakilishwa na mwanasheria machachari, Lisa Bloom.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke mwingine kumshtaki Usher akitaka alipwe takriban dola milioni 20 kwa kumuambukiza gonjwa hilo.

Comments

comments

You may also like ...