Header

Diamond Platnumz na Zari waipokea furaha ya miaka miwili ya ‘Princess Tiffah’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Staa kutoka Tanzania Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz na na mrembo mjasiriamali Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’, leo wameikubuka ile tarehe ya furaha na yenye kufungua ukurasa wa maisha ya familia kwa Diamond Platnumz kama mzazi kwa kupata mtoto wake wa kwanza wa kike ‘Princess Tiffah’.

Kupitia kurasa zao za Instagram, Diamond Platnumz na Zari The Bosslady walimimina furaha na ujumbe wa upendo kwa Tiffah huku wasiache kumtakiwa maisha marefu na kwakuwa ni kumbukumbu ya tarehe ya kuzaliwa na ametimiza umri wa miaka miwili sasa.

It's princess world…happy birthday my one and only👸 @princess_tiffah

A post shared by Zari (@zarithebosslady) on

Pricess Tiffah mbali na kuwa mwenye umri ndogo, ni mtoto maarufu zaidi Tanzania kutokana na kuwa na wafuasi wengi kwenye ukurasa wa Instagram unaowakilisha biashara na maisha yake kwa ujumla ambapo pia anatajwa kuwa mtoto anayeingiza pesa nyingi kwa mujibu wa baba yake mzazi ‘Dizmond Platnumz’ kutokana na mikataba ya kibiashara na ubalozi wa makampuni tofauti yanayomtumia kutangaza bidhaa zao.

Akaunti rasmi ya Instagram ya ‘Tiffah’

Comments

comments

You may also like ...