Header

Stereo awataja Mastaa watakao shiriki kwenye ‘Mpe Habari Remix’

Rapa kutoka nchini Tanzania, James Joseph Masanilo a.k.a ‘Stereo’ anayefanya vizuri na kazi yake ‘Mpe Habari’ aliyomshirikisha Richard Martin ‘Rich Mavoko’, ameuzungumzia muendelezo wa kazi hiyo ya Mpe Habari katika hatua nyingine ya Remix kuwa itafanyika na itawashirikisha wakali wengine ili kuongeza utamu wa kazi hiyo inayofanya vizuri mpaka sasa.

Akipiga stori na Dizzim Online Stereo amesema kuwa ‘Mpe Habari’ ni kazi ambayo imeufikisha muziki wake mbali zaidi na  kukubali kuwa kufanya kwake vizuri ni kutokana na kuwa chini ya promosheni ya viongozi wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi kisha kudokeza kuwa wimbo wa Mpe Habari mashabiki waungoje katika Remix itakayowashirikisha Bill Nas, Jay Moe, na ikasemekana kama utaratibu uliopangwa Rapa Khaligraph kutoka Kenya atakuwepo katika Remix hiyo.

 

Comments

comments

You may also like ...