Header

Moni Centrozone akusanya ladha kwa Pancho na Barakah The Prince

Rapa na hitmaker wa ngoma ‘Tunaishi Nao’ na mmiliki wa lebo ya muziki ya ‘Majengo Sokoni Music Entertainment’ Moni CentroZone ameelezea kikubwa ambacho ni msingi na maana ngoma yake mpya ya ‘Matango Pori’ iliyotayarishwa katika studio za B’Hitz na kumshirikisha Barakah The Prince.

Akipiga stori na Dizzim Online Moni ameshukuru sana wadau na mashabiki kwa mapokezi mazuri ya wimbo wake huo mpya na kubainisha kuwa Barakah ni msanii mkubwa na ushiriki wake katika ngoma yake ipo maana kubwa katika muziki wake hata kukiri kuwa ushirikiano huo umeongeza kitu cha tofauti na kizuri katika ujio wake huo mpya.

Akiongeza kuhusu kuongezeka kwa ladha katika kazi hiyo, Moni amesema kuwa tofauti na wengi walivyotegemea ameamua kufanya kazi na Mtayarishaji Pancho Latino chini yastudio za  B’Hitz kwasbaabu ni kipindi kirefu cha kupungua kwa kasi ya uachiaji wa nyimbo kutoka studio hizo hiyo ilimsukuma kushirikiana na mtayarishaji huyo ili kuongeza miguso yenye ubora pia yeye kuwa sehemu ya wasanii wengi wakubwa ambao wamesha fanya kazi katika studio hizo.

Hata hivyo upande wa utaratibu wa kuachia ngoma, Moni amesisitiza wadau na wote wanaopenda muziki wake wawe tayari kupokea kazi  nzuri na zipo nyimbo nyingi ambazo amesha ziandaa na kusema kuwa kinachoruhusu ngoma kuachiwa ni haina ya mawazo yaliyopo kwenye kila wimbo na miondoko inayoenda sawa na muda wa wanachohitaji mashabiki.

Isikilize na kuitazama kazi yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Matango Pori’.

 

 

Comments

comments

You may also like ...