Header

Rayvanny awagusa tena watu wa hali ya chini ndani ya ‘Chuma Ulete’ huku Producer Zest akijibu tuhuma za wimbo kuvuja

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rayvanny kutoka lebo ya muziki ya WCB, maeachiwa video ya wimbo wake wa ‘Chuma Ulete’ ulitayarishwa na Producer Zest huku video ikiongozwa na Director Elis Mzava. Stori kubwa kuhusu wimbo huu awali kuanza kusikika ni kuwa ulivuja na chumba cha habari haikusika kufanya kazi yake ili kuibuka na ukweli wa jambo hili.

Dizzim Online amezamia mtayarishaji Zest ili ajibu tuhuma za kuwa wimbo huu ulivuja kabla haujatoka rasmi na alifunguka mengi na kuuomba msamaha uongozi wa WCB kwa kitendo cha kuvuja kwa wimbo huo huku akikiri kuwa mwenye makosa kama matayarishaji aliyepewa dhamana ya wimbo huo.

“Nakubali wimbo ulivuja, ni uzembe ambao ulitokea ndo maana na thubutu kuomba msamaha na kuomba msamaha uongozi wa Rayvanny, wanisamehe. Mimi ni mtu ambaye naielewa na nafanya kazi zangu kwa kujiamini na naomba kilichotokea wasinichukulie vibaya, imetokea bahati mbaya tusamehane” Amesema Producer Zest.

Hata hivyo Rayvanny baada ya kuachia wimbo huu wa ‘Chuma ulete’ kwa mujibu wa audio na muonekanao wa kilichoigizwa katika video Rayvanny anaonekana tena katika wazo la wimbo ambalo linazungumzia maisha ya hali ya chini kimaisha kama ilivypkuwa katika wimbo wake wa kwanza kumtambulisha rasmi akiwa katika mkataba na lebo ya WCB ‘Kwetu’.

Comments

comments

You may also like ...