Header

Diamond, Patoranking, Harmonize pamoja London

Diamond na Harmonize wamesafiri wiki hii kwenda nchini Uingereza. Hadi sasa hatufahamu azma ya safari yao hiyo. Lakini kwa picha aliyoiweka Diamond kwenye Instagram huenda tukawa na jibu la safari hiyo.

Staa huyo amepost picha akiwa na staa wa Nigeria, Patoranking wakiteta mambo pamoja na Harmonize na wengine. Kumbuka wawili hao, yaani Diamond na Patoranking wamepanga kuachia wimbo wao mwezi ujao. Kwahiyo huenda wakawa wameenda London ili kushoot video yake.

Ni muda sasa Diamond hajashoot video yake nchini London.

Comments

comments

You may also like ...