Header

FIFA yatangaza orodha ya Wachezaji wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora 2017

Shirikisho la Soka Duniani FIFA Limetoa orodha ya Wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji bora wa kiume 2017, orodha ambayo ina jumla ya Wachezaji 24 kutoka Vilabu mbalimbali Barani Ulaya.

Orodha hiyo imetolewa hii leo Agosti 17 na FIFA itafanyiwa Mchujo mpaka kupata Mchezaji Mmoja ndani ya Wachezaji hao 24. Majina ya nyota hao 24 ni:

Pierre-Emerick Aubameyang (GAB – Borussia Dortmund)
* Leonardo Bonucci (ITA – Juventus/AC Milan)
* Gianluigi Buffon (ITA – Juventus)
* Dani Carvajal (ESP – Real Madrid)
* Cristiano Ronaldo (POR – Real Madrid)
* Paulo Dybala (ARG – Juventus)
* Antoine Griezmann (FRA – Atlético Madrid)
* Eden Hazard (BEL – Chelsea)
* Zlatan  Ibrahimovic (SWE – Manchester United)
* Andres Iniesta (ESP – FC Barcelona)
* Harry Kane (ENG – Tottenham Hotspur)
* Ngolo Kante (FRA – Chelsea)
* Toni Kroos (GER – Real Madrid)
* Robert Lewandowski (POL – FC Bayern Munich)
* Marcelo (BRA – Real Madrid)
* Lionel Messi (ARG – FC Barcelona)
* Luka Modric (CRO – Real Madrid)
* Keylor Navas (CRC – Real Madrid)
* Manuel Neuer (GER – FC Bayern Munich)
* Neymar (BRA – FC Barcelona/Paris Saint-Germain)
* Sergio Ramos (ESP – Real Madrid)
* Alexis Sanchez (CHI – Arsenal)
* Luis Suarez (URU – FC Barcelona)
* Arturo Vidal (CHI – FC Bayern Munich)

Upigaji wa kura unaanza Agosti 21 na kufungwa Septemba 7 mwaka huu, kura zitapigwa na Makocha wa timu za Taifa, Manahodha, baadhi ya Wawakilishi kutoka vyombo vya Habari mbalimbali vitakavyoteuliwa pamoja na Mashabiki kwa Mujibu wa FIFA.

Mchezaji Bora wa Mwaka 2016 wa FIFA alikuwa ni Cristiano Ronaldo ambaye yupo pia katika orodha ya awali ya Mwaka huu.

 

Comments

comments

You may also like ...